Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen tarehe 21 Novemba, 2023. Baada ya kuwasilisha Hati hizo za utambulisho, Mhe. Rais Alexander Van Der Belen amemuahidi ushirikiano Mhe. Balozi Naimi Aziz kwa kipindi chote ambacho atahudumu katika kituo hicho na kumwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Austria. Kwa upande wake, Balozi Naimi alishukuru na kuahidi kushirikiana na Serikali ya Austria katika utekelezaji wa majukumu yake na kuhakikisha uhusiano uliopo unafika hatua za juu zaidi.


